Nyota wa muziki wa Marekani na dada wa aliyekuwa mfalme wa
muziki wa Pop, Janet Jackson amebadili dini kuwa muislamu na atafunga ndoa ya
kifahari na mpenzi wake bilionea wa Qatar, kwa watakaohudhuria kila mmoja
atapewa zawadi ya saa ya Milioni 20.
Dada yake Michael Jackson, Janet Jackson amesilimu kuwa
muislamu na atafunga ndoa ya kiislamu na mpenzi wake bilionea wa Qatar, Wissam
Al Mana mwanzoni mwa mwaka ujao.
Sherehe ya kukata na shoka ambayo inatarajiwa kufanyika
kwenye mji wa Doha, Qatar inatarajiwa kugharimu mamilioni ya dola ambapo
bilionea huyo wa Qatar anataka kuifanya harusi yake iingie kwenye historia ya
harusi bora kuliko zote duniani.
Kwa mujibu wa taarifa za ndani zilizopatikana Janet na
mchumba wake huyo wamepanga kutumia dola milioni 3 kwaajili ya kuwakodishia
ndege za kuwaleta wageni wapatao 500 watakaohudhuria harusi hiyo.
Katika kuhakikisha kuwa wanaifanya harusi yao inakuwa ya
kifahari zaidi, bilionea huyo wa Qatar amepanga kuwazawadia wageni wote
watakaohudhuria sherehe hiyo saa ya kifahari aina ya Rolex yenye thamani zaidi
Tsh, milioni 20. Kila mgeni atapata saa hiyo kama shukurani ya kutumia muda
wake kuhudhuria harusi hiyo.
Janet mwenye umri wa miaka 46 alikutana na Wissam ambaye ni
mdogo kwa miaka takribani 10 mnamo mwaka 2009 wakati Janet alipotembelea nchi
za Mashariki ya kati na kufanya shoo maalumu kwenye nchi hizo.
Janet na Wissam walianza mapenzi yao mnamo mwaka 2010 na
walivalishana pete za uchumba mwaka jana ambapo Wissam alimvalisha Janet pete
ya uchumba ya almasi yenye carat 15.
"Mama yangu alitulea na kutufundisha tuamini kuwa umri
ni namba tu", alisema Janet wakati alipoulizwa kuhusiana na umri wake
mkubwa kulinganisha na Wissam.
0 comments:
Post a Comment