Pages

Labels

Wednesday, November 28, 2012

KAMPUNI YA FASTJET YATUA AFRIKA.


NAIBU Waziri wa Uchukuzi, Charles Tizeba ameagiza Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), kuandaa mazingira mazuri na miundombinu katika Viwanja vya Mwanza na Kilimanjaro kukabiliana na ongezeko la abiria wanaotarajia kuvitumia.
Akizindua safari za ndege za Kampuni ya Fastjet Dar es Salaam jana, Tizeba alisema kuanzishwa kwa safari za ndege za bei rahisi kwa mikoa mitatu ya Dar es Salaam, Kilimanjaro na Mwanza kunatoa changamoto kwa Serikali kuboresha miundombinu kukidhi mahitaji ya ongezeko la wasafiri.
Kuanzishwa kwa safari za ndege za bei rahisi ya Sh32,000 na Kampuni ya Fastjet kunatarajiwa kuvutia abiria wengi zaidi. MSAADA CHINGABLOG

0 comments:

Post a Comment

 

Blogger news

Blogroll

About