Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha
Songa Kibaoni mahala ambako Sharo Milionea alipatia ajali, wamezikimbia nyumba
zao baada ya Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Subira Mgalu kutoa siku moja kwa
waliopora mali za marehemu huyo kuzisalimisha mara moja.
naye mmiliki wa gari ambalo lilikuwa likiendeshwa na msanii maarufu nchini, Hussein Ramadhan ‘Sharo Milionea’ na kupata nalo ajali iliyosababisha kifo chake huko Muheza, Tanga, Mohammed Ismaili maarufu kwa jina la Mudi Suma, ameibuka na kueleza uhusiano wake na marehemu, huku akisema amekubali hasara.

Suma amesema kuwa kabla ya
kuanza safari yake, Sharo Milionea alifika nyumbani kwake mchana na kumweleza
kuwa afya yake haikuwa nzuri.
“Kabla ya kuondoka aliniambia
kuwa hajielewi elewi na kifua kilikuwa kinambana. Nikamshauri asiondoke peke
yake, atafute mtu wa kuondoka naye ambaye atamsaidia kuendesha gari njiani,”
alisema Suma na kuongeza:
“Tulianza kuwapigia simu jamaa
zetu wanne wa kusafiri naye lakini kila tuliyemwambia hakuwa tayari. Ilikuwa ni
changamoto mpaka ilipofika saa 10:45 hivi jioni, akaamua kuondoka peke yake.
Wakati anatoa gari getini kwangu, nikamwambia, basi jaribu kuwa mwangalifu
sana, maana alikuwa kweli anasumbuliwa na kifua. Tukakubaliana kwamba
atakaporudi aende hospitali kucheki afya yake.”
0 comments:
Post a Comment