Friday, December 7, 2012
WANAWAKE WAITISHA MGOMO WA NGONO ITALIA
Serikali ya mtaa wa Sulmona Mjini L'Aquila mkoani Abruzzo, mashariki mwa Italy, imetoa wito kwa wanawake wa eneo hilo kushiriki mgomo wa ngono mpaka uongozi wa jimbo hilo utakapoboresha huduma za afya kwenye wodi ya wazazi katika hospitali ya Sulmona.
Mgomo huo umeazishwa na uongozi wa wodi ya wazazi katika hospitali ya Sulmona,wakishirikiana na wanawake wa eneo hilo katika ngazi mbalimbali, wakiwemo watu wa kawaida na wanasiasa katika ngazi ya mtaa.
kundi hilo la wanawake lilikaa pamoja kisha walikubaliana kufikisha mpango huo kwa ungozi wa Serekali ya mtaa ili kuhakikisha viongozi wanatekeleza wajibu wao katika kuiletea maendeleo hospitali hiyo.
ungozi huo umewataka wanawake wa kigeni kutoka nchi mbalimbli wanaoishi eneo hilo kushiriki katika mgomo huo ili kufanikisha zoezi hilo linalolenga kuboreshwa kwa huduma ya afya katika wodi ya wazazi kwa aliji ya usalama wa vizazi vyao vijavyo.
Mji wa wa L'Aquila ulikumbwa na tetemeko kubwa mwaka 2009, na kusababisha vifo vya watu zaidi ya mia tatu, na kuharibu majengo na miundombinu.
Labels:
yasin
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment