Steven Charles Kanumba (8 Januari 1984, Shinyanga - 7 Aprili, 2012) alikuwa msanii wa maigizo na filamu kutoka nchini Tanzania. Katika historia
ya tasnia ya filamu nchini Tanzania, Kanumba ndiye aliyekuwa msanii wa kwanza
nchini kufanya kazi nje ya nchi na kuweza kuwavuta wageni kutoka nchi
mbalimbali kuja kuigiza Tanzania. Hasa walikuwa Wanigeria kama vile Mercy
Johnson, Emmanuel France, Nkiru Silvanus, Ramsey Nouah, na wengine wengi tu.
Kanumba pia ameweza kuwaleta waongozaji filamu kadhaa was Kinigeria nchini.
Steven alianza masomo yake katika shule ya
msingi yaBugoyi, na kuendela na masomo ya sekondari huko Mwadui na baadae
kupata uhamisho katika shule moja jijini Dar es Salaam iitwayo Dar Christian
Seminary. Alivyomaliza kidato cha nne akaendelea na masomo ya kidato cha tano
na sita katika shule ya sekondari ya Jitegemee ilioko huko huko Dar es salaam.
0 comments:
Post a Comment