Monday, February 4, 2013
SHILOLE AJA KIVINGINE
Msanii wa kizazi kipya kutoka hapa nchini maarufu kama Shilole ambae anatamba na baadhi ya ngoma zake kama Viuno Tucheze, Lawama na hii ya sasa ambayo amempa shavu Q Chief inaitwa Dudu.
Sasa habari kamili kutoka kwa mwanamuziki huyo ni kuwa sasa yuko mbioni kuachia track yake nyingine ambayo ni mpya itakayo kwenda kwa jina la ''Marry Maria'' ambapo humo ndani ameshirikiana na msanii Dully Sykes.
Shilole aliongeza kwa kusema kuwa ujio wa track hiyo ni moja katika kuanza ratiba zake za kufanya show kimataifa ambazo zitaweza kumkuza zaidi kimuziki.
Labels:
yasin
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment