Magazeti katika nchi nyingi za kiafrika yamedanganyika na
stori kwenye tovuti ya kiingereza iliyotolewa kama masihara ikidai kuwa bingwa
wa zamani wa ndondi duniani Mike Tyson amebadili jnsi kuwa mwanamke na uume
wake umeondolewa na kupandikizwa uke.
Magazeti katika nchi za Kiiafrika yale ya udaku na yale yale
ya habari za kitaifa yameingia kwenye mkenge wa tovuti ya Uingereza iliyotoa
habari kama masihara ikidai kuwa Tyson amebadili jinsia kuwa mwanamke.
Magazeti ya udaku na serikali katika nchi za Zambia,
Zimbwabwe na Ghana na bila kuyasahau magazeti yetu ya udaku hapa Tanzania
yaliichukulia habari hiyo kwa umakini zaidi na kuipa nafasi kubwa kwenye kurasa
za mbele za magazeti yao.
Gazeti moja la udaku hapa bongo lilifikia hatua ya kutoa
picha ya mwanaume ambaye lilidai kuwa yuko tayari kumuoa Tyson ili awe mtu wa
kwanza kumega utamu wa bondia huyo bingwa wa zamani wa dunia.
Uzushi wote huu ulianzia kwenye tovuti ya newsbiscuit.com
ambayo ilidai kuwa Tyson amemaliza kufanya operesheni ya kubadili jinsia yake
na uume wake ulionyofolewa na ameuweka kwenye kichupa pembeni ya kitanda chake.
Mwandishi wa gazeti hilo alidai kuwa Tyson amefanyiwa
operesheni hiyo iliyochukua masaa 16 kwenye hospitali iliyoko Los Angeles,
California nchini Marekani.
Mwandishi huyo ili kuwafanya watu waamini stori yake, alidai
kumnukuu Tyson akisema kuwa watu wengi watashangazwa na yeye kugeuka kuwa
mwanamke huku Tyson akidai kuwa atafurahi sana akipata hedhi kwa mara ya kwanza
kama mwanamke.
Habari hiyo ya kzishi ilirushwa tar 30 mwezi uliopita kwenye
tovuti hiyo ya NewsBiscuit lakini ilianza kuzagaa kwenye mitandao baada ya
magazeti mengi ya Afrika kuiona na kuanza kuichapisha kuanzia wiki iliyopita.
Habari hiyo ya kizushi iliwafanya watu wengi waamini kuwa
nguli huyo wa ndondi ni kweli amebadili jinsia wakati si ukweli wa mambo Tyson
ni mwanaume na taarifa hizo hazina ukweli wowote.
Kusambaa kwa uzushi huo kumepelekea Tyson mwenye umri wa
miaka 46, atoe taarifa maalumu kwa vyombo vya habari kuwa habari hiyo ni ya
kizushi na kwamba yeye sio shoga na anautumia vizuri uanaume wake na hana
mpango wa kuwa mwanamke.
0 comments:
Post a Comment