Pages

Labels

Thursday, February 14, 2013

MBUNGE NWA MBEYA MJINI SUGU AKERWA NA STILE YA ROMA.

Msanii wa kwanza kufanya album hapa Bongo na kwa sasa ni mbunge wa Mbeya mjini kupitia tiketi ya CHADEMA, Joseph Mbilinyi a.k.a  Mr II na wengi  hupenda kumuita Sugu ameonyesha wazi kukerwa na ambao ameuimba   ROMA katika ngoma yake ya 2030, Sugu  alichodai ROMA ana kurupuka na hajui anachokifanya.
Akizungumza katika kipindi cha TV wiki iliyopita Sugu  amesema kuwa  msanii huyo anapaswa kuijua misingi ya hip hop na pia Sugu  amemuonya na kumtaka  roma awe muangalifu na anachokiandika na kukitowa  kwa jamii  na sio kukurupuka kama mtu aliyestuliwa toka usingizini.
Sugu amesema yeye ni mfuasi wa hip hop hivyo ukitaka kuwa mwana hip  hop  lazima uzame ndani sana ili ukiandika kitu uwe na uhakika nacho na  si  kufanya kama Roma anavyofanya.Namtahadharisha bwana mdogo awe  muangalifu  na anachokiandika na si kukurupuka hip hop ina misingi yake  na ni  lazima uzame ndani sana maana hip hop ni maisha na ukweli mtupu,  pia  aelewe hip hop ni sauti ya kumkombowa mnyonge sasa unapoimba mambo  ambayo huna uhakika nayo haipendezi maana utakuwa hujaisaidia jamii   husika alisema sugu.
Katika  wimbo  huo wa 2030 kuna kipande kina sema pesa ndio imemaliza vita   yaRuge na Sugu kitu ambacho kimeonyesha kumkera Sugu na kusema kuwaRoma  anakurupuka na kuandika asichokijua maana kwa mstari huo tu umefanya   niaamini kila achoandika hana anachokijua maana mstari huu unanihusu na  hakuna ukweli juu ya alichokiimba.
  Sugu amemtaka Roma kusikiliza nyimbo walizoimba kaka zake ili   zimuongoze katika sanaa yake amesema asikize nyimbo kama za profesa   jay,afande sele,solo thang atagunduwa kuwa zilikuwa ni harakati za   uhakika mfano mdogo amesema asikilize miss Tanzania ya Solo Thang atajua  anachomaanisha.
 Roma alipotafutwa  kujua amejisikiaje baada ya mheshimiwa kuchukizwa na wimbo wake Roma   alisema Sugu ni kaka yake na anaamini kama kuna baya atamuita na   atamrekebisha.




0 comments:

Post a Comment

 

Blogger news

Blogroll

About