Pages

Labels

Monday, January 28, 2013

BREAKING NEWS:LULU URAIANI



Habari zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa Mahakama kuu ya Tanzania imemwachia kwa dhamana msanii wa filamu nchini Tanzania, Elizabeth Michael al-maarufu kama "LULU" aliyekuwa mahabusu katika gereza la Segerea jijini Dar es Salaam alipokuwa akishikiliwa kwa kesi ya kuua bila kukusudia.

Dhamana ya kuachiwa kwa LULU ni pamoja na kuripoti mahakamani kila tarehe mosi ya mwezi na pia wadhamini wawili watakaotoa dhamana ya Tshs Millioni 20 kila mmoja.

LULU aliyekaa gerezani kwa takribani muda wa miezi saba ni mmoja wa wasanii wenye vipaji vya hali ya juu hapa nchini na mmoja kati ya waigizaji mahiri sana wa Tasnia ya BongoMovies.

Karibu tena LULU uraiani.

0 comments:

Post a Comment

 

Blogger news

Blogroll

About