Raia wa Brazili wanaomboleza vifo vya watu mia mbili thelathini
na watatu waliofariki dunia katika ajali ya moto iliyotokea kwenye ukumbi wa
muziki katika mji wa kusini wa Santa Maria.
Maafisa wanasema kuwa wengi wa waathiriwa walikuwa ni wanafunzi
waliokufa baada ya kushindwa kupumua kutokana na moshi mkubwa .
Wengine zaidi ya mia moja wanapata matibabu hospitalini .
Serikali ya Brazil imetangaza siku tatu za maombolezo . Taarifa zinasema kuwa
moto huo ulianza wakati waimbaji wa bendi moja walipowasha fataki.
Maswali sasa yamekuwa yakiulizwa kuhusu usalama wa kumbui za
starehe, huku kukiwa na madai kuwa cheti cha huduma za zima moto kilikuwa
kimepitwa na wakati. Hili ni jana kubwa la moto kuwahi kuikumba Brazil kwa
zaidi ya miongo mitano
Familia za waathiriwa wamekuwa wakiomboleza juu ya majeneza za
jamaa zao katika ukumbi wa mamozezi ambao unatuimika kama jumba la kuhifadhia
maiti.
Kwa sababu ya heshima
kwa waliofariki, serikali iliakhirisha sherehe iliyotarajiwa kufanyika leo
Jumatatu katika mji mkuu, Brasilia, kuadhimisha siku 500, kabla ya kombe la
dunia kungo'a nagna nchini humo mwaka ujao.
Mazishi ya kwanza
mjini Santa Maria yanatarajiwa kufanyika leo , kwa mujibu wa magazeti ya nchi
humo.
Maafisa wa utawala
wametoa majina ya waathiriwa hao,230 huku maiti watatu wakisalia kutotambuliwa.
Kulingana na taarifa
za kituo cha televisheni cha Globo,wengi wa waathiriwa walikuwa kati ya umri wa
miaka16 na 20.
Zaidi ya watu 100
wanapokea matibabu baada ya kushindwa kupumua kutokana na moshi mkubwa.
0 comments:
Post a Comment